Mark 1:9-11

Ubatizo Wa Yesu

(Mathayo 3:13-17; Luka 3:21-22)

9 aWakati huo Yesu akaja kutoka Nazareti ya Galilaya, naye akabatizwa na Yohana katika Mto Yordani. 10 bYesu alipokuwa akitoka ndani ya maji, aliona mbingu zikifunguka na Roho akishuka juu yake kama hua. 11 cNayo sauti kutoka mbinguni ikasema, “Wewe ni Mwanangu mpendwa; nami nimependezwa nawe sana.”

Copyright information for SwhNEN